Sherehe za Nane Nane 2015 Kitaifa zilikua Mkoani Lindi na zilipata heshima ya kuwa na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Waziri wa Ujenzi Dr.John Magufuli ambapo mbali na kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha sherehe hizo pia Rais aliitumia siku hiyo kuzindua rasmi kivuko cha Mtwara.
Kivuko hicho kimepewa jina la Mv Mafanikio na kitakua kikifanya safari zake kutoka Msemo hadi upande wa pili unaoitwa Msangamkuu,Uwezo wa kivuko hicho ni kubeba abiria 600 na Magari 6 mara moja na nimeambiwa pia kivuko hicho kimetumia Bilion 3.3 kwenye utengenezwaji wake.
Picha kwa hisani ya :issamichuzi.blogspot.com
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> Videos