Kama utakuwa unakumbumbuka vizuri ni miaka mitatu imepita toka afariki aliyekuwa mchezaji wa Simba mwenye uwezo wa kucheza namba Zaidi ya tatu uwanjani kwa ufasahaa Patrick Mutesa Mafisango wengi tuna fahamu Haruna Niyonzima alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa marehemu Mafisango.
Team ya millardayo.com ilimtafuta Haruna Niyonzima ambae alikuwa rafiki wa karibu na marehemu Mafisango na lengo kubwa likiwa ni kutaka kufahamu kuhusu Mafisango na familia yake akiwemo mwanae Crespo wapo wapi na wanaendeleaje kuna nini kianendelea toka afariki Mafisango.
“Kiukweli mimi nilikuwa zaidi ya rafiki wa Mafisango kitu ambaocho nakijua au nakifuatilia siwezi kusema familia yake iko vizuri kwa asilimia mia lakini mtu akiwa ana pumua kila kitu kinawezekana Crespo yupo Kigali pale na anasoma na mama yake aliwahi kuja hata hapa Tanzania kwa sababu tuna mpango tulikuwa tuna panga kuhusu kumsaidia”>>>Niyonzima
Marehemu Patrick Mutesa Mafisango alifariki Mei 17 2012 kwa ajali ya gari binafsi alilokuwa anaendesha maeneo ya chang’ombe Dar Es Salaam alikuwa akikwepa baiskeli aina ya guta na ndipo alipopata ajali. Mafisango alikuwa raia wa Rwanda mwenye asili ya Congo.
Zaidi msikilize Niyonzima hapo chini
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos