Maisha ya mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ndani ya klabu hiyo yamezidi kuwa magumu baada ya kocha wa timu hiyo Brendan Rogers kumuweka wazi kuwa hana mipango naye kwa msimu huu.
Balotelli ambaye Liverpool ilimsajili msimu uliopita akitokea AC Milan ya Italia ameshindwa kuonyesha kiwango bora hali ambayo imemlazimu kocha huyo kuingia sokoni kusajili washambuliaji wengine wakiwemo Danny Ings na Christian Benteke.
Hatua aliyofikia Balotelli ni ya kusaka maisha mengine nje ya Anfield baada ya uongozi wa klabu hiyo kuchoshwa na vituko vyake ikiwemo hali ya kutoonyesha juhudi katika mazoeiz na baadhi ya mechi ambazo amepewa nafasi.
Balotelli amekuwa na tabia ya kuendekeza masihara akiwa mazoezini ambapo hivi karibuni alijifunga mwenyewe katika mechi ya mazoezi huku yeye mwenyewe akisimama katika ya uwanja akicheza .
Rogers amefikia hatua ya kumuamuru mchezaji huyo kufanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza ambapo kwa wiki za hivi karibuni amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha timu ya vijana na tetesi kadhaa za vyombo vya habari zimemhusisha na mpango wa kutolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Watford.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos