Ni stori ambayo ilianza kuchukua headline tangu asubuhi ya Agosti 18, 2015 kuhusu ugonjwa wa kipindupindu mitandao mbalimbali imeripoti, sasa saa chache zilizopita ripota wa millardayo.com amefika hospitali ya Mwanyamala kuhakikisha kinachoendelea Hospitalini hapo.
Taarifa kutoka hospitali ya Mwananyamala ni kwamba mpaka sashivi wameshapokea wagonjwa 20 ambao wanahisiwa kuwa na vimelea vya ugonjwa huo wa Kipindupindu.
Kwa mujibu wa Dkt. Ngonyani sasa hivi nimevyoongea tumeshapata wagonjwa 20 wenye vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kati ya hao wagonjwa watatu wamefariki dunia na wagonjwa sita vipimo vyao vimeshatoka na vimethibitishwa kuwa wana vimelea vya ugonjwa vya kipindupindu na waliobaki wanaendelea na matibabu.
“Ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa hatari sana, mgonjwa anapofika hapa hospitalini tumetenga wodi yao maalum kwa ajili ya kupata huduma na kuanza kupata vipimo na pale wanapogundulika kuwa wana vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu, tunawasafirisha kuelekea kwenye Kambi iliyopo Mburahati“- Dk. Ngonyani.
“Sasa ni kuzingatia taratibu za usafi kwanza kunawa mikono unapotoka chooni, pili hakikisha unapokula matunda yaoshe vizuri, tatu mazingira ya nyumbani yawe safi na salama, nne kuepuka na misongamano ya watu hata sehemu zile ambazo mtu amefariki kuweka matanga haturuhusu kufanya hivyo kwa hiyo kuepukana na hivyo vitu basi tunaweza tukaondoa hili tatizo” – Dk. Ngonyani.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos