Leo timu ya LEOTENA kupitia HekaHeka wamezungumzia matukio mbalimbali yaliyowahi kusikilizwa kupitia kwenye hekakeka baada ya kuombwa na wasikilizaji…
Miongoni mwa Hekaheka ambazo wasikilizaji walitaka kujua mwendelezo wake ni pamoja na ya Dada Neema Mwita ambaye alimwagiwa uji na mume wake kisha kulazwa hospitali ya Muhimbili jana alifanyiwa operesheni na yule msamaria mwema aliyejitolea kumpelekea chakula na nguo amejitolea kukaa nae kutokana na mgonjwa kuendelea kumwogopa mumewe anayeishi Musoma.
Kingine ni ile Hekaheka ya mama kumuuza mtoto wake mchanga kwa mmasai kwa kiasi cha laki 1 na kununua kitenge na chips baada ya kuwa na shida ya hela, ishu ya Muhindi kutembea na mke wa mtu, mtoto aliyeibiwa Morogoro,Mwanajeshi aliyekua vitani na kukuta mke wake ana mimba ya mtu mwingine nk.
Pia wameahidi kuendelea kufuatilia Hekaheka ambazo zimewahi kutolewa na ambazo zilikuwa bado zinahitaji muendelezo.
Msikilize mwenyewe Gea Habib na timu yake wakizungumza….
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos