Kamati itakayoamua ikiwa mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius ataachiwa kutoka gerezani, inatarajiwa kukutana tarehe 18 mwezi ujao.
Mwanariadha huyo alizuia kuachiliwa siku ya Ijumaa wiki iliyopita kama ilivyokuwa imetarajiwa.
Waziri wa sheria na haki Michael Masutha amesema kuwa uamuzi wa kamati hiyo ya kutoa msamaha wa kumuachilia mwanariadha huyo, baada ya kutumikia kifungo cha miezi kumi ya kifungo chake cha miaka mitano ulitolewa mapema haina msingi wowote.
Mwaka 2013 Pistorius alikutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi akiwa bafuni nyumbani kwake Pretoria baada ya kumuhisi ni mwizi.
Upande wa mashitaka umekataa rufaa ya hukumu hiyo ukisema kuwa Pistorius anapaswa kuhukumiwa kwa mauaji.
Mawakili wa Pistorius wanatarajiwa kuwasilisha nyaraka zao kupinga rufaa hiyo tarehe 17, mwezi ujao, siku moja tu kabla ya kamati hiyo ya kutoa msamaha kukutana.
BREAKING: another three weeks in jail for #OscarPistorius – his parole review set down for Friday 18 September @eNCA
— Karyn Maughan (@karynmaughan) August 27, 2015
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos