Ni kawaida au rahisi kwa binadamu kuahaidi kitu katika maisha yake ila katika suala la utekelezaji ni wachache sana wanaoweza kutimiza huenda ni kwa makusudi au bahati mbaya wamesahau. August 28 nakusogeza karibu na mchambuzi maarufu Tanzania katika masuala ya soka Edo Kumwembe.
Edo ni miongoni mwa watu wachache waliowahi kuweka ahadi na kuitimiza, tarehe 23 June 2003 ni siku ambayo ipo vichwani mwa wapenda soka wengi kwani ni siku ambayo alifariki uwanjani kiungo mahiri kutokea Cameroon Marc-Vivien Foé katika michuano ya Kombe la Mabara iliyokuwa inafanyika Lyon Ufaransa.
Tukio hilo lilitokea katika mechi kati ya Cameroon dhidi ya Colombia ni siku ambayo kila mpenda soka alishikwa na simanzi akiwemo mchambuzi mahiri wa soka Tanzania Edo Kumwembe, kwakuwa ni mtu wa soka Edo aliamua kuweka ahadi ambayo August 27 imetimiza mwaka mmoja toka ahitimize.
Baada ya tukio hilo Edo aliamua kusema siku atakayo bahatika kupata mtoto wa kiume basi atamuita jina la kiungo mahiri ambaye kwa sasa ni marehemu Marc-Vivien Foé. Kinacho vutia zaidi sio tu kutimiza bali ni ahadi ambayo imetimia baada ya miaka 12. Mwaka jana alipata mtoto wa kiume na kumuita Marc-Vivien Kumwembe.
“Sababu kubwa iliyonifanya nimuite mwanangu jina la Marc-Vivien ni wakati alipoanguka uwanjani na kufariki mwaka 2003 katika michuano ya mabara ilikuwa ni mechi kati ya Cameroon dhidi ya Colombia nilikuwa nyumbani natazama ile mechi”>>> Edo Kumwembe
“kwanza ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona mwanasoka mwenye jina kubwa anaanguka uwanjani na kufariki kwa hiyo pale pale nilisema nikipata mtoto wa kiume nitampa jina la Marc-Vivien nimefurahi nimetimiza ahadi na hata kama angekuwa hai leo hii nakuona ahadi niliyoweka miaka 12 iliyopita nimetimiza angesikia faraja sana” >>> Edo Kumwembe
Hii ni sauti ya Edo Kumwembe
Video ya tukio la Foe
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos