Baada ya kuanza ligi vizuri kwa kushinda mechi mbili za mwanzo na kutoa sare moja, klabu ya Liverpool leo imeanza kuonja joto ya jiwe katika Barclays premier league.
Wakicheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Anfield – Liverpool wamepoteza mchezo wao wa kwanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha 3-0 kutoka West Ham.
Magoli ya West Ham ambao walifungua ligi kwa kuifunga Arsenal – yalifungwa na Lanzini katika dakika ya 3, Noble akaongeza la pili dakika ya 29, Sakho akafunga biashara kwa kushindilia msumari wa mwisho dakika ya 90.
Vikosi vilipangwa hivi: Liverpool: Mignolet, Clyne, Skrtel, Lovren, Gomez (Ibe 78), Can (Moreno 45), Lucas, Milner, Firmino (Ings 61), Benteke, Coutinho.
Subs not used: Sakho, Origi, Bogdan, Rossiter.
Booked: Lucas, Ings, Clyne.
Sent off: Coutinho 52.
West Ham: Randolph, Tomkins, Reid, Ogbonna, Cresswell, Kouyate, Obiang, Noble (Oxford 81), Lanzini, Sakho (Cullen 90), Payet (Jarvis 88).