Kama kungekuwa na uwezo wa kutumia Computer kupika chakula maisha yangekuaje? Au kama simu yako ingekuwa na uwezo wa kupokea ujumbe wa kukutaarifu kuwa chakula chako kipo tayari maisha yangekuaje!?
Nimekutana na stori kutoka Marekani ambako Matt Van Horn na rafiki yake Nikhil Bhogal wametengeneza computer waliyoipa jina ‘June Intelligent Oven’.
June ni oven ya computer inayofikiria na kufanya kazi kama mpishi ‘chef’, oven hiyo inayopatikana kwa dola 1,495 (Million 3,289,000) inatumia computer kutambua ni aina gani ya chakula unataka kupika na kukuelekeza jinsi ya kukipika vizuri zaidi.
>>“hili oven lina uwezo wa kufanya kazi kama computer, simu au hata tablet… kwa uraisi na ufupi ‘June’ ni computer yenye uwezo wa kupika chakula chochote bila msaidizi au mpishi”.<<< Matt Von Horn.
Hili oven halhitaji kuwashwa ili likolee moto lenyewe hufanya kazi kama vile computer nyingine na kizuri zaidi ni kwamba kwa kutumia application yake ya simu iitwayo ‘June Application’ hili oven lina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako kukutaarifu pale chakula chako kikiwa tayari!
Ni mwaka jana tu ambapo Matt na Nikhil waliamua kuacha kazi zao ili kuifanyia kazi ndoto hii, na mwezi uliopita June Intelligent Oven ilizinduliwa rasmi lakini jiko hilo litaanza kusafirishwa mwanzo wa mwaka ujao.
Hizi ni baadhi ya picha za oven la June nilizoweza kuzinasa..
Na hapa chini nimekusogezea video yake ikielezea jinsi ya kutumia oven hio kwa kutumia simu au tablet yako mtu wangu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos