Baada ya Hekaheka ya binti wa kazi aitwaye Sada kupelekwa Oman kufanya kazi za ndani na kufanyiwa unyama na wenyeji wake kias chakurudi akiwa hawezi kuzungumza wala kusikia, leo Wizara ya Mambo ya nje kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu Simba Yahya amezungumza.
Simba Yahya amesema ni kweli wamekuwa wakipata malalamiko mengi kutoka kwa ndugu wa wasichana wanaokwenda huko lakini wengine wakienda huko wanafanikiwa vizuri.
Wameweka mkataba baina ya mwajiri na msichana anayekwenda kufanya kazi, lakini wengi wa hao wasichana hawapati mikataba hiyo kwa kupitia njia za panya.
Amesema pia kwa sasa Wizara hiyo imesitisha kutoa ruhusa ya Wasichana kwenda nchi za Uarabuni kufanya kazi za ndani ..
Msikilize hapa akizungumza na Geah Habib….
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos