Tukiwa bado kwenye headlines za Uchaguzi 2015 kuna taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa hivi karibuni kwamba Mahakama ya kimataifa ya ICC itakuja Tanzania kusimamia Uchaguzi.
Sasa leo ripota wa millardayo.com & Amplifaya alikutana na Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe kupata majibu sahihi kuhusiana na taarifa hizo..‘Kawaida taasisi ili ije kutazama uchaguzi lazima itume barua ya maombi lakini kwa ICC bado hawajaomba na kuna category za taasisi zinataka kuomba kwa hiyo kama itaangukia kwenye sifa basi tutaruhusu lakini kama hiyo taasisi haina sifa haturuhusu, kwa sasa tumepokea taasisi za kimataifa kama 20 na za hapa ndani ni zaidi ya 60’ – Emmanuel Kawishe
‘Kwa hiyo tunaendelea kupokea na tunaendelea kuangalia taasisi zingine zinakosa vigezo tunawaambia taasisi zenu hazijakizi vigezo nendeni halafu mrudi tena kwa hiyo wale wanaokizi vigezo tunawapokea‘ – Emmanuel Kawishe
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos