Ni kawaida sehemu ambayo hutarajia kupokea watu wengi katika kipindi fulani, bidhaa na vitu vingine hupatikana kwa gharama za juu sana, kutokana na mkusanyiko wa watu wengi na kama unahitaji baadhi ya huduma za sehemu hiyo kama hotel, vyakula na vingine kwa urahisi lazima ufanye booking.
Timu ya taifa ya Uingereza imeshaanza kufanya maandalizi ya michuano ya EURO 2016 itakayofanyika Ufaransa, Uingereza imefanya booking ya hotel na kuomba kupata huduma maalum kipindi watakapokuwa hapo, sambamba na gharama ya pound 500 kwa usiku mmoja ambayo ni zaidi ya Tsh milioni 1.6 za Kitanzania kwa chumba.
Huduma watakazopata Uingereza za VIP ni pamoja na huduma ya treni, uwanja wa mazoezi pamoja na ulinzi kwa usalama wa timu yao. Tayari shirikisho la soka Uingereza FA kupitia kwa kocha wa timu hiyo Roy Hodgson limethibitisha kufikia katika hotel ya Auberge du Jeu Paume na kuomba kupata huduma za VIP.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos