Bado siku nne Ligi Kuu soka Tanzania bara ianze, vilabu vilikuwa katika harakati za usajili wa wachezaji na mapumziko ya mechi za kimataifa, lakini jumamosi ya September 12 Ligi Kuu Tanzania bara itaanza rasmi. Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu kuna taarifa hii kutoka TFF.
Kikubwa kutoka katika shirikisho la soka Tanzania TFF ni kukumbusha kuanza kwa baadhi ya michezo itakayopigwa weekend hii, mabadiliko kwa klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba italazimika kutumia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wa Tabora kwa mechi tatu za mwanzo ili kusubiri kumalizika kwa ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba.
“Sasa kutokana na ratiba hiyo timu ya Kagera Sugar ambayo inatumia uwanja wa Kaitaba uliyopo mjini Bukoba, itacheza michezo yake mitatu katika mzunguuko wa kwanza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliyopo Tabora hii inatokana na uwanja wao wa Kaitaba kuendelea na matengenezo”>>> Kizuguto
“Kitu kingine ni kuvikumbusha vilabu kuhusiana na kulipia wachezaji wake wa kigeni dola 2000 ili wapate leseni ya kuwatumia wachezaji hao, hakuna leseni itakayotoka bila kulipia, leseni zote zipo tayari kikubwa watakapo kamilisha zoezi hilo watapata nafasi ya kuwatumia wachezaji hao katika mechi za Jumamosi”>>> Kizuguto
Zaidi msikilize hapa Baraka Kizuguto afisa habari wa TFF
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos