Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo aliitisha mkutano wa vyombo vya habari leo Sept 8 kutoa taarifa ya takwimu ya mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Agosti, 2015.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo alisema..’Mfumuko wa bei wa taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.Mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioshia mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioshia mwezi Julai, 2015′ – Ephraimu Kwesigabo
‘Mfumuko wa bei wa mwezi Agosti, 2015 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.02 ikilinganishwa na asilimia 0.41 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.81 mwezi Agosti, 2015 kutoka 158.78 .mwezi Julai, 2015. Kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangia hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula.Baadhi ya bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na gesi kwa asilimia 2.0 mafuta ya taa kwa asilimia 2.3, mazulia kwa asilimia 1.4, dizeli kwa asilimia 3.8 na petrol kwa asilimia 8.3′ – Ephraimu Kwesigabo
‘Thamani ya shilingi ya Tanzania mwezi Agosti, 2015 ikilinganishwa na mwezi septemba 2015 uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 62 na senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 62 na senti 98 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015‘ – Ephraimu Kwesigabo
‘Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Mfano; Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2015 nchini Kenya umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015′ – Ephraimu Kwesigabo
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza mkurugenzi Ephraimu Kwesigabo
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos