Wakati shirikisho la soka Tanzania TFF likithibitisha kuanza kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara siku ya Jumamosi ya September 12 na kudai mpango wa kuwataka vilabu viwalipie wachezaji wa kigeni dola 2000 upo pale pale. Kwa upande wa Azam FC kupitia kwa afisa habari wake Jafari Iddi Maganga amethibitisha kurejea kwa wachezaji wao.
Awali klabu ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Hisani iliwakosa wachezaji wake wawili Kipre Bolou aliyekuwa majeruhi na Allan Wanga ambaye alifiwa na mama yake mzazi. Wanga amerejea baada ya kukosekana kwa kufiwa na mama yake na kuitumikia timu yake ya taifa ya Kenya.
“Kipre Bolou ambaye alikuwa ameenda Cape Town kwa matibabu, amerejea jana usiku tumempokea na alienda kule kwa ajili ya matibabu yake na tutakuwa naye kwa muda wa mwezi mmoja akiangalia afya yake na wakati huo huo akiandaliwa kucheza katika Ligi Kuu” >>> Jafari Iddi Maganga
“Utaratibu wa madaktari ni kwamba amekwenda wameangalia afya yake na wamesema kuwa hawawezi kumfanyia upasuaji kutokana na hali aliyokuwa nayo lakini wametoa maelekezo kwa madaktari wetu kitu gani kwamba anapaswa kufanyiwa ili aweze kurudi uwanjani”>>> Jafari Iddi Maganga
Ninayo sauti ya Jafari Iddi Maganga
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos