Moja ya matukio ambayo yaliibuka na kutikisa Dunia ilikuwa ni ishu ya Ugonjwa wa Ebola, haikuwahi kushuhudiwa Ugonjwa ambao umesababisha vifo vya watu wengi kama Ebola ilivyofanya ndani ya kipindi cha 2014 na 2015 katika nchi za Afrika Magharibi hasa Sierra Leone, Liberia na Guinea.
Ebola haijasahaulika, Ripoti ziligusa tena Vichwa vya Habari kuhusu ishu ya mwanamke mmoja kufariki mwezi August 2015 Sierra Leone.
Ripoti zinaonesha kuna wagonjwa wengine wamepatikana na maambukizi ya Ebola, na wote walikuwa watu wa karibu na mwanamke mmoja ambaye alifariki kwa ugonjwa huohuo Mwezi August 2015.
Bado kuna wasiwasi wagonjwa wengine kugundulika hasa ndugu na watu wa karibu waliohusika kumuuguza mwanamke huyo aliyefariki.
Pallo Conteh ni Mkuu wa Kitengo kinachoshughulikia Masuala ya Ebola ndani ya Sierra Leone, anasema sababu hasa ya maambukizi hayo unatokana na ndugu wa mwanamke huyo kutotoa taarifa za Ugonjwa na kuendelea kumuuguza nyumbani mpaka hali ikawa mbaya.
Uamuzi uliofanyika sasahivi ni kwamba, Serikali imeweka ulinzi mkubwa kwenye Kijiji ambacho Ugonjwa huo umeibuka, wasimamizi ni Askari na Wanajeshi 1000… wamewekwa kuzunguka Kijiji ili kuhakikisha hakuna mtu anayetoka nje ya Kijiji hicho kusambaza Ugonjwa kwa watu wengine.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos