Tukiwa bado tuko kwenye headlines za uchaguzi 2015 time hii nakusogezea stori kutoka kwa msanii wa Hip Hop Kalapina ambaye ni mgombea wa Ubunge jimbo la Kinondoni Dar es Salaam.
Msanii huyo alikutana na ripota wa millardayo.com leo Sept 9, 2015 na kuzungumza kuhusu pingamzi alilolipata jimboni kwake dhidi ya mgombea mwenza kupitia chama cha Mapinduzi
‘Kiukweli niliwekewa pingamizi na mgombea wa CCM Issa Mohamed akidai kwamba sija dhaminiwa na chama change lakini nikawa nimetoa utetezi wa kutosheleza tu kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi Salim Hassan Msuya wilayani Kinondoni na msaidizi wake anaitwa Victor Muhenge’
‘Lakini kinachoonekana kwa mimi binafsi na hata mtazamo wa chama changu ningependa kusema hiki watanzania wote wajue kwamba pale kuna hujuma manispaa ya Kinondoni kwamba Iddi Hassan anaonekana anashirikiana na watendaji wa pale katika ku engineer hizi pingamizi za namna moja au nyingine’ – Kalapina
‘Kwasababu aliwekea pingamizi wagombea wengi lakini kikuweli hazikuwa pingamizi zenye mashiko na naishukuru ningependa kuishukuru tume ya uchaguzi na mkurugenzi wa tume kwa kuweza kutupilia mbali pingamizi la mgombea wa CCM’- Kalapina
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Kalapina
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos