Jina la Juma Pondamali sio jina geni masikioni mwa waliyowengi katika soka hususani watu waliyokuwa wanafuatilia soka la Tanzania miaka ya 80, Pondamali kwa sasa ni kocha wa magolikipa wa klabu ya Dar Es Salaam Young African.
Ripota wa millardayo.com nilipata nafasi ya kufanya exclusive interview na Pondamali kuhusiana na muziki kwani tumewahi kusikia wakibishana na Peter Manyika kuwa wote wakali, hadi sasa bado hakuna hata mmoja ambaye amekiri kushindwa na mwenzie katika suala la muziki.
Hii inaweza kuwa ngeni masikioni mwako kwani tuliwahi kumsikia Pondamali akisema anaimba muziki wa Bongo fleva, ila kwa hili la kutunga wimbo kwa ajili ya klabu yake ya Yanga ni geni. Kipa huyo mkongwe ametunga wimbo kwa ajili ya Yanga dhumuni likiwa ni kuuza wimbo huo kwa Tsh 500.
“Kuna ngoma ambayo nimeiandaa kwa ajili ya Yanga inaitwa Yanga mbele mbele isirudi nyuma, lengo langu lilikuwa viongozi wakae chini waisikilize ile ngoma wakiona ina vigezo waitangaze kwenye vyombo vya habari ili iuzwe kwa Tsh 500 kwa kila mtu, lengo ni kuwa hela itakayopatikana itumike kujenga uwanja wa kufanyia mazozi kama wa Azam FC wanavyofanyia mazoezi katika uwanja wao”>>> Pondamali
Hili ni wazo Pondamali kawashirikisha viongozi wa Yanga ili ukiuzwa wimbo kwa mashabiki wa Yanga wapate fedha za kujenga uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo pamoja na yeye kupata asilimia ya mgawo katika wimbo huo.
Kama utakuwa unakumbukumbu vizuri Juma Pondamali ni miongoni mwa wachezaji waliyochangia kuiwezesha Taifa Stars kucheza fainali za AFCON mwaka 1980, Pondamali ana umri wa zaidi ya miaka 50 lakini bado anaimba muziki na kufanya kazi yake ya ukocha.
Mengi ameongea hapa Pondamali
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos