Ushindi ni furaha, ushindi ni kitu kizuri… Serena Williams ni staa wa Mchezo wa Tennis, siku chache zilizopita aliibuka na ushindi mzuri kwenye Michuano ya US Open, baada ya kumshinda dada yake, Venus Williams… alifurahia ushindi?
Waandishi wa Habari wakamcheki ikaonekana kama mtu asiye na furaha hivi baada ya Mechi, swali likatoka kwamba nini kimefanya aonekane hana furaha yoyote na ushindi wake?
‘Sasa hivi ni saa tano usiku, kiukweli sijapenda muda huu kuwa na nyie hapa, nilitakiwa kuwa kitandani nimepumzika na ninatakiwa kuamka mapema kwa ajili ya kufanya mazoezi… Sikupenda pia hata kujibu maswali yenu, mnaniuliza maswali yaleyale, yani hata sifurahii chochote hapa kwa kweli‘- Serena.
Kipande chake cha Video hiki hapa mtu wangu..
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos