Panya akiingia ndani ya nyumba na kuanza kusababisha uharibifu wake, hapo ndio ambapo unaanza kuonekana umuhimu wa kufuga paka.
Zaidi ya wafungwa 4,000 wamehamishwa kutoka ndani ya gereza la Pollsmoor lililopo Afrika Kusini baada ya panya kuvamia gereza hilo na kusababisha vifo vya wafungwa wawili.
Mmoja wa viongozi wa gereza hilo Manelisi Wolela, amesema wamelazimika kuwahamisha wafungwa hao hadi pale watakapowaangamiza panya hao.
Amesema panya hao wamesababisha magonjwa kwa wafungwa na kuleta usumbufu mkubwa.
Gereza la Pollsmoor pia limeingia kwenye Historia ambapo Hayati Nelson Mandela aliwahi kufungwa katika gereza hilo wakati akiwa kwenye harakati za kutafuta Uhuru wa South Africa.
Tatizo ambalo limepelekea mpaka Wafungwa kufariki linatokana na magonjwa ambayo yanasababishwa na mkojo wa panya.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE