Ubunifu wa binadamu na maendeleo ya Teknolojia ni vitu ambavyo huwa vinatuletea mambo mapya kila siku, hakuna mtu asiyependa kusifiwa baada ya kufanya kazi nzuri.. ubunifu wa hiki kisiwa ni kazi nzuri ambayo tayari pongezi zimeanza kuwafikiwa wabunifu walioona kuna umuhimu kuwa na kitu kama hiki cha kuvutia.
Tunajivunia uzuri wa Zanzibar yetu, huo ni uzuri kwenye kisiwa cha asili kabisa.. taarifa ikufikie kwamba wapo waliowaza kutengeneza kisiwa kinachohama kwa kutembea juu ya maji kama ilivyo meli au Boti.
Najua kwamba Dunia inavitambua pia visiwa vilivyotengenezwa na binadamu ikiwepo Palm Island, ambacho kiko Dubai… lakini Dunia inatambulishwa pia kwenye Kisiwa ambacho kimebuniwa na wataalam wa Kampuni ya Migaloo ambao wanadili sana na kutengeneza Boti za kifahari.
Ubunifu huu utasogezwa kwenye Maonesho maalum ya Monaco Yatch Show na tayari watu wenye pesa zao wameonekana kuvutiwa sana na hii kitu, kwa hiyo tayari ni biashara ambayo inatarajia wateja wa nguvu kabisa any time kuanzia sasahivi !!
Ukiangalia nje mpaka ndani Kisiwa hiki kinavutia, na kina mahitaji yote muhimu kwa mtu anayehitaji kuishi ndani yake, kwenye vilivyomo unaambiwa mpaka Beach za nguvu kabisa zipo ndani !!
Ubunifu huo wa nguvu huu hapa pia kwenye video mtu wa nguvu, teknolojia ina mazuri yake ya kuvutia kila siku yani !!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE