Kingine kikubwa kwenye vichwa vya habari Tanzania sasa hivi ni pamoja na kifo cha waziri wa nchi, ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma, Mama Celina Kombani kutokana na maradhi ya Saratani.
Mwanzoni zilitoka taarifa za kifo chake tu lakini haikuzungumzwa ilipoanzia ambapo September 25 2015 Michael ambaye ni ndugu wa karibu wa marehemu aliongea na millardayo.com na kusema ‘Baada ya kura za maoni alirudi nyumbani Dar akasema amechoka tukajua ni malaria tukampeleka hospitali akapata vipimo ikasemakana kwamba ni malaria na akaendelea na matibabu mpaka siku ya mwisho alipoelekea India kufanya check-up tu kama mtu wa kawaida ili arudi Tanzania aendelee na kampeni’
‘Alipokwenda India ndio hali ikabadilika na akafariki, mwili wa marehemu ulitarajiwa kuwasili Tanzania saa tisa na nusu alasiri September 25 2015, nakumbuka mara mwisho alikuwa ni mtu mwenye afya nzuri na wala hakuna mtu ambaye alitegemea katika leo litatokea hili, Marehemu ameacha watoto watano (wakiume wanne na wakike mmoja)’ – Michael
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Michael