Kuachana na mtu uliyekuwa unampenda inauma sana na kujaribu kuweka mawasiliano na ex boyfriend ama ex girlfriend wako inaweza kukuletea stress kubwa sana licha ya kila mtu kuwa na namna yake ya kusonga mbele… mara nyingine huwa inatokea wapenzi wa zamani kuendelea kuwasiliana kama marafiki kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.. je hii ina athari gani?
Nimekutana na stori moja ambayo ningependa kushare na wewe mtu wangu, kuna utafiti umefanyika na Chuo Kikuu cha Hawaii kwa ushirikiano na Chuo cha Ohio State University ambao wenyewe unasema kuwa asilimia kubwa ya wapenzi wengi wa zamani hufuatiliana kupitia mtandao wa Facebook yani Facebook stalk! Sababu kubwa inasemekana ni kushindwa kukubali kuwa uhusiano umefika mwisho!
Iko hivi mtu wangu… ulikuwa na mpenzi wako ambaye kwa bahati mbaya mambo hayakwenda vizuri mkaachana, na pengine ulimpenda sana na kumsahau inakupa tabu kutokana na vitu vingi ambayo mmefanya pamoja wakati wa mahusiano yenu… ili kujua mpenzi wako anafanya nini na nani unaanza kufuatilia kila anachokifanya kwa kutumia Facebook, kwahiyo akitoka unajua alitoka na nani,alikwenda wapi na saa ngapi… kila atakachokifanya mpenzi wako wa zamani wewe uko nyuma kufuatilia!
Utafiti huo umesema kwamba wanawake na wanaume kati ya miaka 18 hadi 42 hutumia zaidi ya masaa 4 kwa siku kumchunguza ex- girlfriend ama ex-boyfriend wake kupitia Facebook kujua anafanya nini, wapi na nani na ametumia muda gani na huyo mtu! Sababu zinazowafanya watu wengi kuwa na stress kubwa ya mapenzi!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE