Asubuhi huwa ni time ya kuchambua stori kubwa zilizokamata kurasa za magazeti kwenye #PowerBreakfast @CloudsFM, ninazo zote zilizosikika leo baadhi zikiwa…
Edward Lowassa ataja mambo 13 ya kwanza atakayofanya kwa siku 100 akipata nafasi ya kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya 5, UKAWA waja na azimio la Kawe kumbana Kikwete, Mahujaji wasimulia vifo vya Mecca, Wassira amesema anamuweka kiporo Bulaya.
Ndege ya JWTZ yaanguka porini, ahadi tano za Rais Kikwete mzigo kwa Rais ajae, Edward Lowassa atangaza neema kwa mapolisi ni miongoni mwa vipaumbele vyake 11, Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa asema UKAWA wataunda Katiba mpya, Jaji Damian Lubuva akimbia ofisi kwa kukerwa na madai ya wizi wa kura.
Askari wawili wa JWTZ waliokuwa kwenye mafunzo maalum ya kijeshi wamepotea kwenye bahari ya Hindi baada ya ndege yao ya mafunzo kuanguka maeneo ya kisiwa cha Mbudya kilichopo nje kidogo na jiji la Dar es salaam.. juhudi za kuwatafuta askari hao bado zinaendelea.
Jeshi la Polisi Bukoba limewakamata watu 16 wanaodaiwa kuhusika kwenye tukio la kuchoma moto Makanisa… NACTE imeviamuru vyuo vyote kufungwa hadi mwezi November ili kutoa fursa kwa wanafunzi wote kushiriki ipasavyo kwenye zoezi la kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu October 25.
Rufaa iliyokatwa na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona kupinga adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kutoka leo… NEC kwa mara ya kwanza imeruhusu waandishi wa habari kufika katika maendeo ya kupiga kura, kuhoji wapigaji kura na wasimamizi kwenye Uchaguzi Mkuu October 25.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye sauti hii hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE