Umeme umekua ukikatika na kukaa kwa zaidi ya saa kumi na mbili kwenye maeneo mbalimbali Tanzania ikiwemo Dar es salaam, sasa yote hii majibu yake yametolewa na Mkurugenzi wa TANESCO Injinia Felichesmi Mramba kwenye Exclusive Interview na millardayo.com
- Dar es salaam katikati ya jiji kuna mradi wa umeme unaojengwa kwa kushirikiana na serikali ya Finland ya kujenga kituo kipya cha umeme katikati ya jiji kitakachokamilika Novemba 2015 hivyo maeneo ya Ilala, Makumbusho na katikati ya jiji yamekua yakizimiwa umeme sababu ya kazi inayoendelea.
- Arusha kuna kituo kikubwa cha Njiro kimejengwa upya ambapo mjenzi amemaliza kazi yake ila kinachoendelea ni kuunganisha kituo kipya na laini zinazosambaza umeme Arusha.
- TANESCO imeanza kuwasha mitambo baada ya gesi kufika Dar es salaam hatua kwa hatua kadri presha inavyofika kwenye bomba, mtambo wa kwanza uliwashwa September 17, mitambo imekua ikiendelea kufanyiwa kazi na kuwasha hadi leo.
- Ikifika tarehe 9 au 10 October 2015 tatizo la kukatika kwa umeme linaweza kuwa limepungua kwa kiasi kikubwa ila tarehe 20 October tatizo ndio litakua limemalizika kabisa nchi nzima.
- Kilichoandikwa kwenye gazeti kwamba TANESCO haina pesa ndio maana hakuna umeme ni UONGO.
- Wananchi wawe na subira, bomba la gesi lilikua jipya na uwashaji mitambo hauwezi kufanywa yote kwa mara moja au kwa siku moja, ni lazima uende taratibu lasivyo kazi tuliyoifanya kwa miaka miwili tunaweza kuiteketeza ndani ya wiki moja.
- Mitambo mingine ikiendelea kuwashwa hivi karibuni Dar es salaam haitaathiriwa tena na kukatika kwa umeme ila mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya itapata mkato kidogo mpaka tarehe 7 October, baada ya tarehe 7 Wananchi wataona mabadiliko wenyewe.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE