Bado ni ngumu kutabiri matokeo ya mechi za Ligi Kuu mbalimbali duniani, kutokana na vilabu vingi kuwa vimejiandaa kiasi kwamba zile timu ambazo tunaziona kuwa bora kuliko nyingine huwa zinapoteza michezo katika timu ambazo huenda ukawa unaona ni kibonde kutokana na jina la timu hiyo kutokuwa maarufu masikioni mwa watu.
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania imekutana na kipigo cha goli 2-1 dhidi ya klabu ya Sevilla, mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa Estadio R. Sanchez Pizjuan, FC Barcelona ambayo inaendelea na mechi za Ligi Kuu Hispania bila nyota wake Lionel Messi ambaye yupo nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nane kutokana na kuwa majeruhi.
Dakika ya 52 ya mchezo Michael Krohn-Dehli alianza kwa kuiandikia goli la kwanza klabu yake ya Sevilla wakati ambao FC Barcelona wanajipanga namna ya kusawazisha goli hilo, Vicente Iborra dakika 6 baadae akafunga goli la pili kwa upande wa Sevilla na kuzidi kuidhoofisha FC Barcelona. Neymar pekee ndio alipata nafasi ya kuipatia FC Barcelona goli la kufutia machozi dakika ya 74 kwa mkwaju wa penati.
Video ya magoli Sevilla Vs FC Barcelona
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE