July 01 2015 story ya Boss wa Twitter kujiuzulu ilichukua headlines kwenye Vyombo Vikubwa vya Habari pamoja na Mitandaoni pia, ambapo Boss wa wakati huo, CEO Dick Costolo alilazimishwa kujiuzulu kutokana na Kampuni hiyo kutofanya vizuri Kibiashara.
Baada ya Costolo kuachia nafasi yake, mmoja ya waanzilishi wa Twitter, Jack Dorsey alikabidhiwa kuwa Mkurugenzi wa muda wakati ambao wanafanya mchakato wa kumpata Boss mwingine… Bodi ya Wamiliki wa Twitter imetangaza rasmi kwamba uamuzi walioufanya ni kumchagua Jack Dorsey kuendelea kuwa Boss wa Twitter.
Wamiliki wa Twitter hawakuridhishwa na Mwenendo wa Biashara yao ambapo Ripoti zinaonesha Twitter ina wastani wa watumiaji Milioni 316 kwa Mwezi huku idadi kubwa wakijitoa na kuacha kutumia Mtandao huo.
Our work forward is to make Twitter easy to understand by anyone in the world, and give more utility to the people who love to use it daily!
— Jack (@jack) October 5, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB , Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE