Kama utakuwa mfuatilia hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazoenea na kuchukua nafasi kubwa katika mitandao mbalimbali ile ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda kufariki na ile ya mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamunyange kuwekewa sumu ambapo taarifa hizo si za kweli.
Kwa mujibu wa msemaji wa Serikali Assah Mwembene akiongea leo Octoba 6, 2015 mbele ya waandishi wa habari alisema...‘Kuna taarifa nyingi sasa hivi zinaendelea kuenea katika mitandao ya kijamii ambazo si nzuri sana kulikuwa na taarifa za kuzusha kuhusu kifo cha Dkt Abdallah Kigoda na wengine mpaka leo wanasema kwamba TV ya serikali imeshatoka yaani TBC wameshatoka taarifa kwamba ameshafariki taarifa hizo sio za kweli‘ – Assah Mwembene.
‘Mimi ndio msemaji mkuu wa Serikali kwa hiyo niliposema hili kupitia TBC kwamba Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda ni kweli ni mgonjwa amelazwa katika hospitali iliyopo nchini India anaendelea na matibabu… Kumzushia kifo sio jambo zuri‘ – Assah Mwembene.
‘Lakini pia kuna wengine waliozusha habari za Mwamunyange kuwa alipewa sumu taarifa zote hizo si taarifa sahihi kwa hiyo Serikali inafanya uchunguzi kuhusiana na matukio hayo yote, kusema kweli wote waliohusika na kuandika hizo taarifa watachukuliwa hatua tayari tumeshapata mitandao iliyohusika kuandika hizo taarifa muda ukifika tutatangaza rasmi kuwa waliohusika ni akina nani‘ – Assah Mwembene.
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza msemaji wa Serikali Assah Mwembene akizungumzia hizo taarifa mbili.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE