Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita? Ninazo hapa chini baadhi ya stori zilizoweka headlines kwenye kurasa za magazeti Tanzania leo 7 October 2015, kama zilikupita unaweza ukacheki na hizi nyingine kufidia.
Kingunge akurupuka kifo cha Mtikila, Lowassa mikoa 26 mikutano 104, Magufuli mikoa 20 mikutano 180, Lowassa na Magufuli waishukia TANESCO, NEC matatani, Dk. John Magufuli atikisa ngoma ya Arusha asema wanaokata umeme kipindi hiki watajuta na Lowassa kusamehe mikopo ya Chuo Kikuu.
Umoja wa Mataifa UN umesema tafiti zilizofanywa kutokana mbio za kisiasa nchini hazitoshi kwa 100% kusema nani atakayeshinda uchaguzi mkuu wa Serikali ya awamu ya 5, Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imegundulika kuwa miongoni mwa taasisi 17 za umma zinazojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye ugawaji wa zabuni zake.
Wagombea Urais wa vyama vya Siasa CHADEMA na CCM wamezungumzia tatizo la umeme na kuahidi kuwashughulikia wahusika endapo mmoja wao ataingia Ikulu, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amshukuru Rais Kikwete kwa juhudi alizozifanya kunusuru machafuko ya kisiasa nchini Kenya, Watanzania watatu wauawa kwa ujambazi Uganda.
Familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila imehusisha kifo cha Mchungaji huyo na harakati za kisiasa, msemaji wa familia apingana na kauli ya Polisi huku wanafamilia wakitaka Serikali kuangalia upya mazingira ya kifo chake na mwili wa marehemu kuagwa leo saa tano asubuhi kwenye viwanja vya Karimjee.
EWURA imetangaza kushuka kwa bei za nishati, Petroli, Diesel na mafuta kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na aliyedaiwa kusambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama General Davis Mwamunyange amenusirika kifo kwa kunyweshwa sumu akamatwa na Jeshi la Polisi, upelelezi wa kina unaendelea dhidi yake.
Mkoa wa Dodoma unaandaa sherehe ya kumuaga Rais Kikwete itakayoambatana na shughuli za kitaifa za uzimaji Mwenge kwenye siku ya kumbukumbu ya Mwl. Julius Nyerere tarehe 14 October mwezi huu.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast kwa kubonyeza play hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE