October 7 ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilishuka dimbani kucheza mechi ya hatua za awali za kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018. Huu ulikuwa ni ufunguzi rasmi wa kuanza kwa hatua za awali za mechi hizo. Taifa Stars inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa ilianza kampeni yake kwa kucheza na timu ya taifa ya Malawi.
Taifa Stars ambayo ilikuwa na nyota wake wote hadi wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini na Congo, imeingia ikiwa na rekodi ya kufanya vizuri katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Nigeria kwa kutoka bila kufungana na mabingwa hao wa zamani wa Kombe la mataifa ya Afrika. Taifa Stars katika Viwango vya FIFA ipo nafasi ya 136 wakati Malawi wakiwa nafasi ya 101.
Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam imemalizika kwa timu ya taifa ya Tanzania kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0, magoli ya Taifa Stars yalifungwa na Mbwana Samatta dakika 19 na Thomas Ulimwengu dakika ya 22 . Taifa Stars itacheza mechi ya marudiano na timu ya taifa ya Malawi Jumapili ya October 11 mjini Blantyre Malawi.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE