Ni kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona watu fulani kutoka tasnia fulani kupewa tuzo za heshima kwa kutambua mchango wao katika sekta husika. Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA, kimetangaza rasmi kufanyika kwa tuzo hizo Jumatatu ya October 12 huku mgeni rasmi akiwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Tuzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka kwa mwaka huu zitakuwa tofauti kidogo kwani zitatumika kumuaga Rais Jakaya Kikwete na kumpa tuzo ya heshima kwa kuthamini mchango wake katika kipindi cha miaka 10 aliyokuwa madarakani.
Awali tuzo hizo zilikuwa zifanyike October 8 ila kwa sasa zitafanyika Jumatatu ya October 12, tuzo zitatolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, baadhi ya tuzo zitakazotolewa siku hiyo ni tuzo 10 za wachezaji bora waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, tuzo 5 kwa viongozi wa michezo, taasisi iliyochangia kukuza michezo katika kipindi cha miaka 10 na tuzo ya heshima kwa Mh Rais.
Mwewnyekiti wa TASWA Juma Pinto na katibu mkuu wa TASWA Amir Mhando wamethibitisha hayo kufanyika katika mkutano na waandishi wa habari.
“kwa wale ambao hamfahamu tutatoa Tuzo kumi kwa wachezaji wale ambao wamefanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi ila tumeangalia nje ya Tanzania yaani Afrika Mashariki lakini tutatoa tuzo kwa viongozi watano waliochangia kukuza michezo, tuzo zote hizo zitatolewa na Rais Kikwete”>>> Amir Mhando
Sauti ya Juma na Amir Mhando
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.