Timu ya taifa ya Tanzania inayofundishwa na kocha Charles Boniface Mkwasa akisadiana na Hemed Morocco wamefanikiwa kusonga mbele katika harakati za mechi za awali za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018 itakayofanyika Urusi.
Licha ya kupoteza mchezo kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Malawi mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa Kamuzu mjini Brantyre Malawi, Taifa Stars imefanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata kwa matokeo ya jumla ya goli 2-1 baada ya mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Kwa sasa Taifa Stars itakutana na mtihani mgumu wa kucheza na timu ya taifa ya Algeria katika hatua inayofuata ili iweze kufuzu katika hatua ya makundi, huu ni mtihani kwa Taifa Stars ambayo ipo nafasi ya 136 katika viwango vya FIFA wakati Algeria wapo nafasi ya 19 katika viwango hivyo. Taifa Stars itacheza na Algeria mwezi November lakini bado TFF hawajatangaza rasmi tarehe ya mechi hiyo ila inaaminika kuwa November 14 Dar Es Salaam na kurudiana ni November 17 Algeria.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.