Mara nyingi nchi zilizoendelea huaminika zaidi kufuata uzazi wa mpango tofauti na nchi zinazoendelea kwa sasa, ingawa wataalam wa mambo ya uzazi wanashauri wazazi kufuata uzazi wa mpango lakini wapo wengine ambao hukiuka utaratibu huo.
Cheryln Prudham mwenye umri wa miaka 33 amejaliwa kuwa na watoto 12 na bado hajafikiria kuwa huenda ujauzito aliona sasa utakuwa ni wa mtoto wa mwisho.
Mwanamke huyo raia wa Ujerumani akihojiwa na televisheni ya Ujerumani alisema anashukuru Serikali yake kumsaidia kila mwaka na haoni kama ni kosa kuwa na watoto wengi.
Amesema kwa mwaka yeye na mume wake Rob wamekuwa wakitumia kiasi cha zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya kutunza watoto wao na wamekuwa hawana tatizo lolote katika kuwatimizia mahitaji yao.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.