Kama ulikua hujui, mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Dar es salaam Young African Danny Mrwanda kwa sasa yupo katika klabu ya Lipuli FC ya Iringa inayoshiriki Ligi daraja la kwanza, amemalizana na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita na alijiunga na Lipuli FC ya Iringa baada ya kutaka kuwa huru.
Wengi walikuwa wanataka kufahamu ni nini kilichomfanya Danny Mrwanda kwenda kucheza Lipuli FC ya daraja la kwanza…… ni kweli anaelekea kustaafu soka? uwezo wake umeisha? amekosa klabu yoyote ya Ligi Kuu inayomuhitaji katika Ligi Kuu Tanzania bara? majibu yote yako kwenye sentensi zinazofata…
“Kwanza uelewe ningetaka kucheza Ligi Kuu Tanzania nisingeshindwa kucheza katika timu yoyote, kuna timu nyingi tu zilikuwa zinanihitaji. Lipuli mimi nimekwenda kwa sababu maalum sitaki nibanwe kwa kipindi hiki kwani wakati wowote naondoka, mimi nipo Lipuli kama sehemu ya mazoezi ili muda wangu ukifika wa kuondoka, naondoka nikiwa katika kiwango kizuri, kwani muda wowote kuanzia hivi sasa naenda Malaysia”>>> Danny Mrwanda
Mrwanda amewahi kutamba katika vilabu kadhaa vya Ligi Kuu Tanzania bara kabla ya kuamua kwenda kujikita katika Ligi Kuu Vietnam kwa zaidi ya miaka 4. Kwa sasa Danny Mrwanda ambaye awali kulikuwa na stori kuwa anaenda Thailand, amethibitisha kuwa na mipango ya kwenda kucheza soka katika Ligi Kuu Malaysia muda wowote kuanzia hivi sasa.
Hii ni sauti ya Danny Mrwanda mtu wangu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE