Good Morning mtu wangu, ni asubuhi nyingine ambayo siku zote lazima ianze na uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM, ninazo zote kubwa za leo kutoka kwenye kurasa za magazetini Tanzania.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama NLD na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Dk. Emmanuel Makaidi amefariki dunia katika hospitali ya Nyangao, Lindi chanzo cha kifo chake ni matatizo ya shindikizo la damu… Ujenzi wa barabara ya juu maeneo ya TAZARA, Dar es Salaam unatarajiwa kuanza mwezi ujao chini ya kampuni ya Japan ujenzi ambao utagharimu zaidi ya Bilion 100, unategemea kutumia miezi 35 na nia ni kuboresha miundombinu ya barabara nchini.
Mgombea Urais kupitia ticket ya CHADEMA, Edward Lowassa ameituhumu Tume ya uchaguzi NEC kwa kumpotosha Rais Kikwete, asema Tume ya Uchaguzi NEC ina kazi kubwa sana kuhakikisha Uchaguzi Mkuu October 25 unafanyika kwa amani huku akiitaka Tume hiyo isifanye mambo yatakayoharibu uchaguzi mkuu.
Wachambuzi wa Kisiasa Tanzania wamesema idadi kubwa ya wapigaji kura sio msingi mkuu wa kuhakikisha ushindi wa Uchaguzi Mkuu October 25 kwani sera nzuri zinazoweza kutekelezwa ndio msingi wa ushindi wa Uchaguzi, taarifa za kuhisi sio majibu sahihi kuhakikisha ushindi wa Uchaguzi Mkuu October 25 kwani pia wengi walio na vitambulisho vya kupiga kura huvihitaji kwa ajili ya mambo yao binafsi hivyo, takwimu za idadi wa wapiga kura ni takwimu nyingine na pia watu watakaojitokeza kupiga kura ni takwimu nyingine.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE