Ni headlines baada ya headlines inawezekana ulikuwa na maswali mengi kuhusiana na kauli ya tume ya Uchaguzi kuhusu kusimama mita 200 pale unapomaliza kupiga kura siku ya tarehe 25, 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Octoba 21, 2015 wakili Peter Kibatala..’Maombi yetu kimsingi yalikuwa yana maombi makuu mawili namba 1 tulikuwa tunaiomba mahakama itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 cha sheria ya Uchaguzi ili kuona kama kifungu hicho kinatoa katazo au hakitoi katazo kwa wapiga kura au raia wengine wenye shauku ya kufuatilia au kukaa karibu na kituo cha kupigia kura au baadae kinachobadilika kuwa kituo cha kuhesabia kura nje ya umbali wa mita 200‘ – Peter Kibatala
‘Maombi yetu sisi ni kwamba sheria kifungu husika kinaruhusu watu kukaa umbali huko nje ya kituo katika umbali huo na ndio tulivyotoa maombi yetu mahakamani tumeomba pia mahakama itoe tamko kwahiyo ndio hoja tulizowasilisha mahakamani na kesho tunaendelea kesho tarehe 22, 2015′ – Peter Kibatala
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE