Mara nyingi wasafiri huwa wanakuwa na imani yote kwa Dereva, wakati safari inaendelea unaweza kukuta abiria wanasinzia, wengine wako busy wanapiga story.. wengine wanachat, ni kwa sababu wana imani kwamba safari iko kwenye mikono salama ya Dereva.
Kuna wakati kumbe hata ajali zinatokea sio kwa sababu ya uzembe wa Dereva au ubovu wa gari, nimekutana na video kwenye mtandao wa Youtube.. Dereva kapoteza fahamu katikati ya safari Jiji la Guizhou China, kaanguka chini huku gari ikijiongoza yenyewe.
Basi lilikuwa na jumla ya watu kama 20 hivi, likaanza kuyumba ikabidi kijana mmoja aliyekuwa amekaa siti ya jirani asogee kwenye sterling kuingoza gari ili angalau isimame salama na kuepusha ajali.
Dereva wa Basi hilo alifariki wakati wakiwa njiani kumkimbiza Hospitali, lakini basi lilisimama salama na hakuna abiria yeyote aliyeathirika kwenye tukio hilo.
Video hii hapa ilirekodiwa kwa Camera ya CCTV ndani ya basi hilo.
Kipande kingine cha Video hiki hapa kikionesha tukio lote lilivyokuwa.
https://www.youtube.com/watch?v=J28IfOGZCxQ
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.