Mara nyingi watu wanaotumikia Vifungo Gerezani huwa hawana uhuru wa kushiriki mambo mengi ikiwemo kusoma Shule, nimekutana na hii stori toka Kenya ambapo watu 16 ambao wanatumikia Kifungo wamepata nafasi ya kusoma na kuhitimu Diploma ya Theology.
Watu hao wanatumikia Kifungo Gereza la Kapsabet lililopo Wilaya ya Nandi, wameishukuru Serikali kwa kupewa nafasi ya kusoma Theology na baada ya kutunukiwa vyeti vyao Ijumaa ya October 23 2015 .
Theology ni elimu ambayo inahusisha masuala ya Dini kwa hiyo Wafungwa hao watakuwa wanatoa Huduma ya kuhubiri Magereza mbalimbali ikiwemo hilo la Kapsabet ambamo wamefungwa wenyewe.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.