Hekaheka October 26 2015 imegusa yaliyojiri kwenye Vituo vya kupigia Kura… moja ilitokea Zanzibar jana ambapo mke na mume walipishana, mume anataka chama kingine mke naye anataka chama kingine..
Mwisho wa mzozo wao ilikuwa ndoa kuisha kwenye Kituo cha kupiga Kura, mume akachukua kalamu na karatasi na kuandika talaka hapohapo !!
Kisa kingine kimetokea Mwananyamala Dar ambapo mmoja wa wasimamizi alihisiwa ameenda chooni kuficha karatasi za Kura, baadae watu waliokuwa kwenye foleni walimletea mzozo lakini baada ya Askari kuingilia kati walichunguza na kugundua hakukuwa na ukweli wowote kuhusu Msimamizi huyo kuficha Kura.
Hekaheka ziko kwenye sauti kutoka kwenye show ya ‘Leo Tena‘ Clouds FM Radio hapa mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE