Tukiwa tumemaliza headlines za Uchaguzi Mkuu 2015, mwigizaji Frank alijitokeza kugombea Ubunge jimbo la Tabata Segerea kupitia tiketi ya ACT-Wazalendo lakini kutokana na kura zake kuwa chache hakufanikiwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Akiongea na ripota wa millardayo.com mwigizaji huyo alisema…’Nilikuwa mgombe ubunge jimbo la Segerea kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, ingawaje sikuwa mshindi lakini naimani wamempokea vizuri mshindi Bonnah Kaluwa…! Na nimekubali matokeo’– Frank
‘Bado naonekana nina deni kwa wale walionipigia kura kama wawakilishi wa wana Segerea, hivyo kuna baadhi ya mambo yaliyo ndani ya uwezo wangu nitayafanya kwa wananchi wangu‘- Frank
‘Kulikuwa na changamoto nyingi, ingawa najipanga upya mwaka 2020 kugombea tena…! Ili kuweza kusaidi matatizo kama tatizo la maji, ujasiriamali, ajira, michezo na afya‘-Frank
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Frank
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE