Good Morning mtu wangu, ni jumatatu nyingine na kama kawaida lazima tuanze na Uchambuzi wa Magazeti @CloudsFM. Inawezekana baadhi ya stori kubwa kwenye kuperuzi imekupita, nimezisogeza zile zote za leo hapa chini.
Saa 72 zabaki za Magufuli kuwashughulikia mafisadi na majizi, Mawaziri waweweseka, nusu yao hawana nafasi Baraza la Mawaziri la Dk. John Magufuli… Ibrahim Lipumba ashtushwa na kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa ZEC Zanzibar akidai mwenyekiti huyo hakufanya haki kwa kutowashirikisha Makamishna wengine.. Bidhaa Zanzibar zapanda bei baada ya meli zinazosafirisha bidhaa hizo kupunguza safari za kwenda visiwani huko kutokana na hali ya kisiasa iliyopo visiwani humo.
Wakati sintofahamu juu ya hali ya Zanzibar ikiendelea, Rais Jakaya Kikwete ameiamuru ofisi yake kusaidia kufanikisha mazungumzo kati ya mgombea Urais wa CUF Maalim Seif na Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama General Davis Mamunyange… NEC imesema sababu ya Kura laki nne kuharibika ni elimu ya uraia na ya mpiga kura kutokuwafikia wananchi kwa usahihi.
Uchaguzi wa Ubunge kwa majimbo ya Handeni na Arusha mjini umepangwa kufanyika tarehe 12 December 2015 ambapo Mkurugenzi wa NEC jana amesema hivi karibuni watatangaza kuanza kwa kampeni baada ya kupitisha majina ya wagombea, Majimbo ya Lushoto na Ulanga Mashariki uchaguzi kufanyika tarehe 22 November lakini kampeni sehemu hizo zimeshaanza huku majimbo ya Ludewa na Masasi mjini taratibu zake kutangazwa hapo baadae.
Aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini kwa ticket ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ametangaza kukata rufaa kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompatia ushindi mgombea wa Chama cha CCM kwenye nafasi hiyo.
Stori zote kwenye audio hapa mtu wangu, kutoka #PowerBreakfast ya CLOUDS FM.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.