Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kauli yake imeingia katika headlines usiku wa November 5 baada ya kuanza kuizungumzia klabu yake ya zamani ya Manchester United ya Uingereza.
Staa huyo wa Real Madrid amekiri kuwa Man United ina kazi nzito ya kufanya ili irejee katika kiwango chake cha juu kilichozoeleka, Ronaldo ambaye amekiri kuumia akiona Man United haifanyi vizuri kama zamani aliwahi kucheza Man United katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2009 na alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu Uingereza na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Kiukweli nataka kuona Man United ikiwa katika kiwango cha juu kama ilivyokuwa zamani, kwa mfano Sporting Lisbon ilikuwa ni klabu yangu ya kwanza na napenda kuona ikiwa katika viwango vya juu, kuhusu kurudi Man United nipo vizuri hapa hakuna anayejua kitu cha mbele katika maisha kama nilivyosema awali mimi bado na mkataba na Real Madrid najisikia furaha hapa”>>> Cristiano Ronaldo
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.