Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili ya November 8 itacheza mchezo wake wa pili wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na USM Alger ya Algeria mjini Lubumbashi. TP Mazembe watacheza mchezo huo wa pili wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga USM Alger katika mchezo wa kwanza uliyochezwa Algeria kwa jumla ya goli 2-1.
Kuelekea mchezo huo klabu ya TP Mazembe wamefanya kitu tofauti kidogo na timu nyingi za Afrika ambazo tumezoea kuona zikihusishwa na imani za kishirikina, hususani zikiwa zinaelekea katika mechi ngumu kama hiyo, TP Mazembe walikusanyika na mashabiki wao na mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi Chapwe na kwenda pamoja kufanya ibada kanisani ili kuomba mungu wapate matokeo mazuri.
Kitendo walichofanya TP Mazembe inaripotiwa kuwa huwa ni kawaida yao kufanya ibada hususani wakiwa wanaelekea katika mchezo mgumu, hii inashangaza kidogo kwani kwa kumbukumbu za karibuni haijawahi kufanywa na klabu za Tanzania zaidi ya kusadikiwa kufanya ushirikina katika mechi zao.
Hii ni sauti ya ibada hiyo waliofanya TP Mazembe na mashabiki wao
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.