Ikiwa bado siku kama 60 kuweza kufikia January ya mwaka 2016 wakati ambao vilabu kadhaa barani Ulaya vitakuwa vikihusishwa kusajili wachezaji kutokana na kuwa ni wakati ambao dirisha dogo la usajili litakuwa limefunguliwa, klabu ya Liverpool ya Uingereza tayari imeanza kunyemelea huduma ya mshambuliaji wa kibrazil Alexandre Pato.
Alexandre Pato ambaye amewahi kuchezea klabu ya AC Milan ya Italia kwa sasa anacheza klabu ya Sao Paulo kwa mkopo akitokea klabu ya Corinthians na anatajwa kurudi Corinthians mwezi January 2016 ila klabu hiyo inataka kumuuza kutokana na kutaka kupunguza mzigo wa gharama kwa klabu.
Kupitia kwa Rais wa klabu ya Corinthians Roberto De Andrade amethibitisha kutaka kurejea kwa mshambuliaji huyo mwezi January ila wamemuweka sokoni, licha ya kuwa amesema hakuna klabu ambayo imeomba kujua bei ya mshambuliaji huyo ambaye anatajwa kufikia thamani ya euro milioni 25 na amefunga jumla ya magoli 26 kwa mwaka 2015 katika mashindano yote aliyocheza.
“Ndio tunataka kumuuza Pato, tunajua ni ugumu kiasi gani utakuwa kwa upande wetu wakati atakaporejea na sina uhakika kama tutafanikiwa kumuuza ila Corinthinans bado haijapokea ombi kutoka katika klabu yoyote ya kutaka kujua bei ya mchezaji huyo ila wakala wake anafanya mazungumzo na vilabu vya Ulaya kwa ajili ya uhamisho”>>> Roberto De Andrade
Hata hivyo uchunguzi uliyofanywa na vyombo vingi vya habari za michezo ni kuwa klabu ya Liverpool ndio inahusishwa kwa karibu kutaka kumsajili Alexandre Pato hususani kauli ya Rais wa Corinthians Roberto De Andrade kutaja kuwa wakala wa mshambuliaji huyo anafanya mazungumzo na vilabu vya Ulaya.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.