Asubuhi yako inaendaje mtu wangu? Inawezekana uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita, pengine ulikuwa busy na hukuzipata zote kwenye PowerBreakfast, nilizozirekodi zote ziko hapa.
Rais Dk. John Magufuli aibukia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es salaam ajionea uchakavu wa vifaatiba na ukosefu huduma, amlipia mgonjwa matibabu na kumuondoa Mkurugenzi Mkuu wa hosptali hiyo, avunja bodi na kuteua na asononeshwa na wagonjwa kulala chini.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema raia wa Kenya hawafai kuwa duniani kwasababu ni wezi sugu, licha ya kupata elimu nzuri wanapora lakini hawaadhibiwi na watu wa namna hiyo hawatakiwi Zimbabwe.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Mohamed Shein na Mgombea mwenzake wa CUF Maalim Seif jana walikutana kwenye kikao cha faragha kwa takribani saa tano lakini hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu kilichojadiliwa kwenye kikao hicho, kikao hicho kiliwahusisha pia Marais wastaafu wa Zanzibar na Jamhuri wa Muungano, Ali Hassan Mwinyi na Amani Karume.
Baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kushuhudia utoaji mbovu wa huduma na kuchukua hatua ya kuvunja bodi ya Ukurugenzi wa hosipitali hiyo, Rais Dk. John Magufuli amemuondoa Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Hussein Kidanto… Dk. Kidanto amerudishwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine, na kutokana na kuondolewa kwake Rais Dk. John Magufuli amemteua Prof. Lawrence Mseru kukaimu nafasi hiyo mpaka pale atakapomteua mtu mwengine.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, HESLB imewapangia mikopo wanafunzi 40,836 baada ya kukidhi vigezo vyake, mikopo hiyo imetolewa siku moja baada ya Baraza la Vijana wa CHADEMA, BAVECHA kuipa bodi hiyo saa 72 kutoa majibu ya kwanini wanafunzi 82% wa vyuo vikuu wamekosa mkopo wa masomo kwa mwaka wa 2015-2016.
Unaweza pia ukasikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini kwenye hii sauti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE