Kuelekea michuano ya mataifa ya Ulaya yatakayofanyika mwaka 2016, shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza mpira maalum kwa ajili ya kutumika katika mashindano hayo, mpira wa utaotumika katika mashindano hayo ya mataifa ya Ulaya kwa mwaka 2016 umetengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya kijerumani ADIDAS.
Mpira huo maalum wa Euro unaoitwa kwa jina la kifaransa la ‘Beau Jeu’ ambapo kwa kiingereza unatafsiriwa kwa jina la ‘the beautiful game’ unatajwa kufanana na mpira (Brazuca) uliotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 iliyofanyika Brazil . Mpira wa ‘Beau Jeu’ ulitengenezwa kwa zaidi ya miezi 18.
Michuano ya Euro 2016 itafafanyika Ufaransa lakini ADIDAS imekuwa ikipokea tenda ya kutengeneza mipira ya mashindano hayo kwa miaka mingi sasa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.