Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti November 16, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Baada ya ukimya hatimaye SUMAYE ajitokeza, asema walishindana na dola siyo CCM kwenye Uchaguzi Mkuu #Gazeti #MWANAHABARI #NOVEMBER16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Matukio ya Ujambazi kama ule wa ‘Panya Road’ yaibuka Dar, watumia risasi kuvamia maduka maeneo ya Yombo ‘Jet Lumo’ #GazetiDIRA #NOVEMBER16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Umoja wa UVCCM wamesema muda wa kuoneana haya umeisha, kama kuna viongozi wasaliti CCM wanapaswa kuwekwa hadharani #GazetiUHURU #NOVEMBER16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Zaidi ya Wabunge wateule 200 wamejisajili tayari kwa kuhudhuria vikao vya Bunge la 11 Dodoma litakaloanza kesho #GazetiUHURU #NOVEMBER16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Walimu Shule ya Msingi Logalombogo iliyopo Simiyu wamegeuza wanafunzi vibarua wao, wanawalimisha mashamba na kuwapa ujira mdogo #UHURU NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Zomba Mkoa wa Ruvuma ameuawa kikatili baada ya kuua watoto wawili #GazetiUHURU #NOV16 >>https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Rushwa yakithiri Mkoa wa Pwani, baadhi ya Askari wageuza mradi wa kujiingizia kipato badala ya kusimamia majukumu yao #GazetiUHURU #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Askari wa Usalama barabarani akiri kupokea rushwa ya Tshs. 10,000 Tanga, asema alipewa kama shukrani #UHURU #NOV16 >>https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Gari la Polisi waliokuwa doria lapinduka Singida, Askari mmoja afariki na wengine watatu kujeruhiwa #UHURU #NOV16 >>https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Kipimo cha X-ray Hospitali ya Wilaya Igunga kimekuwa kibovu kwa miaka mitatu, wananchi walalamikia uzembe wa Watendaji #GazetiUHURU #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Edward LOWASSA amesema hajakata tamaa, ameshindwa pambano na si vita, ajipanga upya ila agoma kuelezea mikakati yake #MTANZANIA #NOVEMBER16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Wasomi na wachambuzi wa masuala ya siasa wametoa angalizo kwa wabunge wakisema wanatarajia kuona bunge lililokomaa #MWANANCHI #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mbunge Mteule Dk. Harrison MWAKYEMBE amesema Waziri Mkuu atateuliwa na Rais Dk. JPM na sio taarifa zinazozagaa mitandaoni #MTANZANIA #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Vijana wa jimbo la Lulindi, Mtwara wamesusia uchaguzi mdogo wa Mbunge jana kutokana na kushindwa kwa mgombea wao LOWASSA #MWANANCHI NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Uongozi wa Soko la samaki Feri umesema wameanza ukarabati wa soko hilo ili kudhibiti moshi usiingie Ikulu #MTANZANIA>https://t.co/tSRGmg2VsC

Kamati kuu ya CCM imemwengua spika wa Bunge la 9 Samuel Sitta kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Uspika na kuteua wengine watatu #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Polisi Geita wanawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha aliyekuwa M’kiti wa CHADEMA Mkoani humo Alphonce Mawazo #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Msichana mmoja amelazwa Hospitali ya Mkoa Singida baada ya kumwagiwa mchuzi wa maharage ya moto, chanzo ni wivu wa mapenzi #MTANZANIA #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia UKAWA, LOWASSA amesema atashiriki kikamilifu katika siasa na kuweka wazi ataendeleza mapambano #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Wanawake wajawazito wametakiwa kufanya mazoezi ili kujiepusha na upasuaji wakati wa kujifungua #MTANZANIA #NOV16 >>https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Hospitali ya Aga Khan Mwanza imeanza kuwafanyia uchunguzi wa saratani mbalimbali wanawake na kuwataka wajitokeze kujua afya zao #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Katibu mkuu wa Chama cha TADEA, Shibuda amevitaka vyama vyote vya siasa vilivyosimamisha wagombea Z’bar kurudia uchaguzi #MWANANCHI #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Wachimbaji wadogo wa madini Kahama wameingiwa hofu baada ya uvumi kuwa wenzao 6 waliofukiwa siku 42 zilizopita bado wapo hai #MWANANCHI NOV
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mbunge Mteule Mussa ZUNGU amesema atafurahi kama Wabunge watampitisha Job NDUGAI kuwa Spika wa Bunge #JamboLEO NOV16>https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Hospitali ya rufaa KCMC, Moshi ipo kwenye mchakato wa kuanzisha kitengo cha upasuaji wa moyo #MWANANCHI #NOV16 https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Ufukwe wa Oysterbay kufanyiwa ukarabati ili uwe kitovu cha biashara na utalii, Ni baada ya miaka mitatu ijayo #MWANANCHI #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
TAMISEMI imesema shule za Sekondari 100 pekee TZ ndizo zenye maktaba, hali hiyo inaathiri ajira za wakutubi #MWANANCHI #NOVEMBER16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mauaji ya Ufaransa yaliza dunia nzima, raia wa nchi mbalimbali wameandamana huku Mataifa yao yakipeperusha bendera nusu mlingoti #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Watahiniwa 397,250 wanaanza mitihani ya kidato cha pili leo TZ, mtihani huo unamalizika Novemba 27 #JamboLEO #NOV16 >https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Makocha na wachambuzi wa soka wamemtetea kocha wa Taifa Stars, MKWASA wakidai hapaswi kuangushiwa mzigo kutokana na matokeo hayo #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
LOWASSA ataja sababu 4 za kumpinga Rais Dk.MAGUFULI, asema atabaki kuwa ngangari ndani ya UKAWA na kuendeleza mapambano #NIPASHE #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Manispaa ya Temeke imeendelea na ukaguzi wa usafi nyumba kwa nyumba kubaini wanaochafua mazingira kwa makusudi #MTANZANIA #NOVEMBER16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mkuu wa Mkoa Tanga amewaambia watendaji wa Serikali kama watashindwa kwenda na falsafa ya ‘Hapa kazi tu’ wafungashe virago mapema #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Chuo kikuu cha UDSM kinatarajia kuzindua shule mbili zitakazofundisha sayansi za afya pamoja na Kilimo #NIPASHE NOV https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Kipindupindu chatinga Kiteto Manyara, watu wanne wa maeneo tofauti walazwa kwa ajili ya matibabu #JamboLEO #NOV16 >https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Ktk hali isiyo ya kawaida, Wanafunzi wa Shule ya msingi Sofu iliyopo Chalinze wanadaiwa kujibu ‘SIJUI’ maswali yote kwenye Mtihani #JamboLEO
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Spika mstaafu Pius MSEKWA amesema spika wa Bunge la 11 anatakiwa awe mwadilifu, mwenye busara na atakayefuata kanuni za Bunge #NIPASHE NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Kauli ya’Hapa kazi Tu’ imepokelewa visivyo na baadhi ya watu baada ya vijana wanaojihusisha na uhalifu kuitumia wanapofanya uhalifu #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mtaalam wa upasuaji wa uti wa mgongo na magonjwa ya mfumo wa fahamu kutoka hosp. ya Apollo, India ametua Dar kuendesha huduma hiyo #NIPASHE
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mbunge wa Kyela, Harison Mwakyembe amesema nafasi ya Uwaziri mkuu haipatikani kwa kupendekezwa kwenye mitandao ya kijamii #TzDAIMA #NOV16
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mkazi wa Mbinga, Ruvuma ameuawa kisha mwili wake kuchomwa moto na wananchi baada ya kudaiwa kuwaua watoto wawili na kumjeruhi mmoja #TzDAIMA
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Akinamama 30 wajitokeza kupimwa Saratani ya kinywa na matiti ktk Hospitali ya Ocean Road bila malipo #RaiaTZ >>>https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Mkurugenzi wa Kituo cha LHRC, Dk. Hellen Kijo BISIMBA apelekwa India kwa ajili ya kuendelea na matibabu #RaiaTZ >>>https://t.co/tSRGmg2VsC
— millard ayo (@millardayo) November 16, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.