Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya Wabunge wapya zipelekwe katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya Wagonjwa wanaolala chini, limetekelezwa.
Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, baiskeli za kubebea Wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vimefungwa Jumapili ya November 22 2015 na kisha Rais mwenyewe atakwenda Hospitalini hapo Jumatatu ya November 23 2015 viwe vyote vimefungwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokosa vitanda.
Wadau mbalimbali walichangia kiasi cha shilingi milioni mia mbili ishirini na tano (225) kwa ajili ya kugharamia hafla ya Wabunge baada ya uzinduzi wa bunge la kumi na moja Dodoma lakini Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.
TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI DR. MAGUFULI ALIVYOAGIZA MBELE YA WABUNGE.