Zile stori ambazo zinamuhusu staa wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kurejea katika klabu yake ya zamani ya Manchester United bado zinazidi kuingia katika headlines, moja kati ya watu wanaofanya wengi waamini huenda staa huyo akarejea Man United ni majibu yake akiulizwa kuhusu mpango huo huwa anajibu majibu ambayo bado yanaacha maswali vichwani vya watu kuwa staa huyo atarejea Man United siku moja.
November 22 kocha wa klabu ya Manchester United muholanzi Louis van Gaal amedhiirisha Ronaldo yupo katika mipango yao na sio kama ambavyo wengi wanafikiria kuwa staa huyo kurejea Man United ni mawazo ya mashabiki wa klabu hiyo pekee, bali hata Van Gaal na anakiri kuwa hakuna kocha duniani ambaye hataki kuwa na Ronaldo katika kikosi chake.
“Anacheza nafasi ya winga anacheza kwa haraka na kufunga magoli sifikirii kama kuna kocha katika hii Dunia ambaye hamuhitaji Ronaldo, bilashaka tutakapoanza kusajili tutaangalia wachezaji wote sio Ronaldo pekee hivyo tusubiri tuone” >>>Louis van Gaal
Ronaldo aliondoka Man United mwaka 2009 na kujiunga na Real Madrid kwa dau la pound milioni 80, licha ya kauli ya Van Gaal haiwezi kueleweka moja kwa moja, Man United wanatajwa kuandaa dau la pound milioni 60 kumrejesha nyota wao huyo Old Trafford hususani katika dirisha la usajili la majira ya joto la mwaka 2016 kwani Ronaldo anatajwa kutokuwa na maelewano mazuri na Benitez.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.