Bado headlines za Real Madrid kufungwa goli 4-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa Santiago Bernabeu dhidi ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona zinzazidi kuchukua nafasi, mchezo huo wa El Clasico ambao umeonekana kuwatawanya mashabiki wa Real Madrid pande mbili tofauti, wengine wakiamini kufungwa ni hali ya mchezo ila wengi wao wanaamini ni mbinu mbovu za Rafael Benitez.
Kabla ya mchezo wa El Clasico kuchezwa kulikuwa na stori kuwa Real Madrid kama watafungwa na FC Barcelona walikuwa wanatajwa kuwa huenda wakamfukuza Benitez na nafasi yake ya itachukuliwa na kocha wa kikosi cha wachezaji wa akiba wa Real Madrid (Castilla) Zinedine Zidane kitu ambacho Zidane amekanusha hadi sasa kurithi nafasi hiyo na kuwa yeye ni kocha na anafurahia nafasi yake ya kukifundisha kikosi cha akiba.
“Mimi ni kocha wa Castilla lakini Benitez ni kocha wa kikosi cha kwanza cha Real Madrid na mambo yako sawa na ninafuraha kuona tunafanya vizuri na kikosi changu cha Castilla dhidi ya wapinzani wetu ambao tumekuwa tukicheza dhidi yao, kiukweli kama kocha nina mengi ya kujifunza siku hadi siku na bado sijakamilisha vyote” >>> Zidane
Hata hivyo kauli ya Zidane bado haijitoshelezi kuhusu yeye kutorithi nafasi ya Rafael Benitez ila wengi wanasubiri majibu ya Rais wa Real Madrid Florentino Perez ambaye jioni ya November 23 ameitisha kikao cha bodi na baada ya hapo ataitisha press conference na waandishi wa habari, hivyo tunaweza kusikia chochote kikitokea kwani hali sio nzuri katika jiji la Madrid, mashabiki bado wamechukizwa na mbinu za Benitez za timu kujihami zaidi kuliko kucheza mpira.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.